Saturday 3 December 2016

MACHINGA WAZUA BALAA JIJINI MWANZA .

Baada ya kuwepo kwa fununu ama taarifa zisizokua rasmi kuwa jiji la mwanza linataraji kuanza kufanyiwa usafi wa maeneo yake yote hasa katikati ya jiji hatiamaye usemi huo umetimia.
 
Machinga wanafanya biashara zao katikati ya jiji hasa eneo la MAKOROBOI wamekua katika wakati mgumu kuanzia jana siku ya Ijumaa baada ya kutolewa tamko rasmi wakitakiwa kuondoka eneo hilo.
 
Hali hiyo imekua mbaya zaidi kuanzia asubuhi ya siku ya leo Jumamosi tarehe 3/12/2016 baada ya halmashauri ya jiji kuanza harakati hizo kwa kasi zaidi.

Wakazi wa jijini hapa wamekua katika hofu kubwa kutokana na kuwepo taarifa zisizokua rasmi kuwa machinga hao wamepanga kuibua vurugu kubwa sana kwa wale wote watakao husika kuwaondoa katika eneo hilo.
 
Kitendo kinachowafanya wakazi wa jiji kuwa mbali kabisa na eneo hilo na kushindwa kupata mahitaji yao ya kila sku.
 
Guta66.blogspot.com imefka eneo hilo na kujionea utata huo,na kubahatika kuongea na baadhi ya Chinga hao waliotoa onyo kali kwa viongozi wa jiji na kutohtaji kwekwa kwa sura na picha zao katika chombo hiki cha habari za kila siku.

Edwin84 alipata nafasi pia ya kuonana na askari wa jiji waliokua katika mazingira hayo na walipotakiwa kuongea juu ya suala hili hawakua tayari kutokana na suala la kiusalama na kudai kua wao sio wasemaji rasmi.
                                

No comments:

Post a Comment

edwinmalima88@gmail.com

Comments system

[facebook] [disqus] [facebook][disqusss] [blogger][facebook] [facebook][blogger] [disqus][facebook][blogger] [blogger][disqus][facebook]

Disqus Shortname